PROMO ZINAFELI, SIJASHIKWA MKONO_MATARE bmj4life

Msanii wa muziki wa kisasa kutoka nchini Rwanda Joshua Matare maarufu kama Bishop Matare anasema kwamba muziki wake sio wa kutafuta kiki za huku na huku bali ni kupasha ujumbe tofauti kwa jamii kulingana na mambo yale yanayohitajika katika jamii.

Akihojiana na mwandisha wetu, Matare amewaelekeza vidole vya lawama wasanii wadogo wanaojidai ustaa wakati hawajafikia viwango vizuri vya kuwapa vipato na mafaniko katika maisha yao.
"Tatizo kubwa ni kwamba unakuta msanii ambaye bado anapambana kujulikanisha muziki wake,lakini anafell lyke he?she want spend a whole day at home doing nothing!...just watching movies..playing games.. hapo huwa anakosea sanaa juu inapofika industry ya muziki wetu,msanii anapaswa kuwa na kazi zingine ambazo zitamsaidia kupata gharama ya studio, mahitaji mengine katika maisha ikiwemo mavazi n.k juu bado hatujafikia level nzuri kwamba msanii akitoa ngoma anaanza kuhesabu." Amesema BMJ4LIFE.

Matare ama Bmj4life kama anavyopenda kujitunga siku hizi ni miongoni mwa wasanii ambao wanatunga mashairi ya kinyarwanda lakini pia wakijaribu kuchanganya na kiswahili kama lugha ambayo inaeleweka kote katika nchi za ukanda wa afrika mashariki.Anaamini kwamba wasanii wakuu ndio wanawopaswa kuweka mkakati sana ili kuuvusha mipaka muziki wa Rwanda ambao bado uko nyuma kiasi kulingana na muziki wa Tanzania,Kenya na Uganda.

BMJ4LIFE MATARE(mwenye kofia ya RANGERS) NA MSHIKAJI WAKE.

"Msanii mdogo hawezi lawumiwa .Bali wasanii wakubwa ambao wana resources za kutosha, wamepata madili mengi katika muziki lakini uwekezaji wao katika biashara hii bado mdogo sana.Unakuta msanii anaingiza miliyoni kumi kwa mfano,lakini kuwekeza atatumia miliyoni moja tu katika biashara ambayo imemwezesha kuwa miongoni mwa mamiliyoneya! hapa ni kuchezea kazi!! itatuangamizi na sisi wasanii wadogo.Wao ni kama road block ambazo zinatukataza kwenda mbele! madili yote yanaenda kwao lakini kupanua soko la muziki wa nyumbani kwa ujumla ni kitu ambacho wengi wao hawajaelewa vizuri lakini kuna imani juu mindset zimeanza badilika." kasema Matare.

Bmj4life ambaye anafanya na wimbo wake wa Winyendereza (Audio) baada ya Madamu ambayo inapatikana viooni, amegusia pia sababu zinazombania njia na jambo la kwamba jina lake halijawa kabambi katika muziki wa Rwanda.Ametaja kutokuwa na meneja wala mtu wa kusaidia kifedha na kimawazo pamoja na masomo yake ya chuo kikuu kama sababu ambazo zimekuwa chanzo cha ngoma zake kama Nipagawe,Mumbwirire, Mu buryohe n.k kutotambaa sana nchini.

"Unajua muziki ni kitu ambacho mtu hawezi kufanya to the full kama yuko mwenyewe! sema tu mi nimepambana kinoma.hakuna mtu amenipa support yoyote ya fedha katika muziki,iwe mzazi,ndungu ama rafiki!Kuanzia mwishoni mwa 2016 ambapo nimefanya Mumbwirire mpaka sasa,nagharamia studio,promo,nauli za kwenda huku na huku....lakini hata kama ni kidogo utakuta muziki wangu umepenya mpaka Burundi, Tanzania, Kenya na kwingineko... channels za kujulikanisha muziki siyo radio na TV tu! promosheni mamboleo inafanyika sana mitandaoni.Ningekua na back up yoyote, ningekua nimeshapiga hatua na kuwa maarufu nationally at least lakini sijajuta kwa sababu jina langu linapofika ni sawa na nguvu zangu binafsi.Sijashikwa mkono, promo nikipanga mara nyingi zinafeli juu budget inakuwa limited." Ameongeza Matare.



Bmj4life
Matare ni miongoni mwa wasanii wachache ambao wana vipaji kwamba ukisikia sauti yake na jinsi anavyoingia katika biti lolote utakubali kwamba wanaweza.
"Mimi naamini kwamba muziki ni kazi lakini pia inabidi kuwa na support ama kuwa na uwezo kwa mtu mwenyewe wa kugharamia studio,promo n.k ili kuweza kufaulu.naomba sana wasanii wa Rwanda kwa ujumla na wasanii wadogo kwa upekee kutafuta kazi zingine za kufanya ili kujiweza...kitu muhimu ili kujiweza kifedha...tusije kwa muziki kwa kuiga wengine.lazima tuwe na vipaji" Amesema Matare.

Anaomba kila mtu kumfutilia katika mitandao yote ya kijamii na kuonyesha upendo kwa kusambaza kazi zake ili zifikie kila mtu.

Facebook:
Bmj Matare Joshua Bmjforlife
Instagram:matarebmj4life_250
Twitter:@matarejoshua
You tube:Bishop Matare
LinkedIn:Bishop Matare.

Leave your comment