TANZANIA: Vanessa Mdee Baada Ya Money Mondays, ‘Ningependa Usikiliza Albamu Ya Grace Matata’

 

Msanii Vanessa Mdee baada ya kuachia albamu yake ya kwanza Money Mondays amesema angependa kusikiliza albamu mpya kutoka kwa Grace Matata kwa sasa.

Muimbaji huyo wa ngoma ‘Wet’ amesema kuwa amekuwa akifuatilia muziki wa Grace Matata na umekuwa wenye kumvutia hivyo angependa kuupata ukiwa katika albamu (package).

“Nilikuwa nasikiliza kazi za Grace Matata juzi kati, ladha zake ni tofauti sana, ningependa kusikiliza albamu nzima kutoka kwake ana kitu fula hivi akikuimbia na gitaa unatulia,” Vanessa ameiambia Clouds TV.

Utakumbuka kuwa Grace Matata alishatoa albamu yake ya kwanza iliyokuwa inakwenda kwa jina la Nyakati.

Muimbaji huyo amemtaja Maua Sama kama msanii mwingine ambaye angependa kusikiliza albamu kutoka kwake. Pia Vanessa Mdee ameeleza kuwa EP ya Mimi Mars itatoka mwisho mwa mwaka huu ikiwa na nyimbo sita.

Courtesy: bongo5.com

Leave your comment

Other news