TANZANIA: Anachokifikiria Ray C Kuhusu Diamond Platnumz

Story ambayo imeshika headlines kwenye mitandao ya kijamii ni ya msanii mkongwe katika game ya Bongo Fleva, Ray C baada ya kupost picha ya Diamond Platnumz na kuandika ujumbe kwa mashabiki wa muziki wanaomponda Diamond Platnumz.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Ray C ameandika caption inayosema;

“Mi naumiaga sana nikiona huyu mtoto anasemwa semwa kila siku! Amefanya mapinduzi makubwa sana huyu mtoto! kama una macho unaona! Muziki wa Tanzania umefika mbali sana sababu ya watu kama hawa! Nigeria wanafika mbali sana kwa sababu wanasapotiana lakini Bongo sijui kwanini tunapenda. Kuzodoana! Kushushana! Kuchukiana! Dah!! Yani huyu alieanzisha hizi social media Mungu amlaani!!” – Ray C.

Maneno haya yanatafsiriwa kuwa yanawalenga wale wote ambao hawaoni mafanikio aliyoyaleta Diamond Platnumz katika muziki wa Bongo Fleva na kuufanya ujulikane kimataifa zaidi na wamekuwa wakimuangalia Diamond katika upande ambao anakosea tu.

Source: millardayo.com

 

Leave your comment

Other news