TANZANIA: Vanessa Mdee Apiga Mil. 40 Mauzo ya Money Mondays Ndani ya Mwezi Mmoja

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ameendelea kuwadhihirishia wasanii wenzake kuwa album zinalipa ni suala la kujiamini na kujipanga kibajeti hii ni baada ya kutangaza mauzo ya album yake tangu aiachie mwezi Januari mwaka huu.

Vanessa Mdee amesema mpaka sasa ameuza nakala zaidi ya elfu 4 na kila nakala moja anaiuza kwa shilingi elfu 10 ambapo kwa mahesabu ya haraka haraka ameingiza zaidi ya shilingi milioni 40 ndani ya mwezi mmoja.

Namshukuru Mungu tumeshauza nakala zaidi ya elfu nne za CD ya #MoneyMondaysTheAlbum kwa sasa tupo Zanzibar kuendelea na mauzo. Asanteni Sana kwa support yenu. Let’s get to 10,000 copies in less than a month. Usinunue CD ya #moneymondays isiyokuwa na sticker ya TRA." ameandika Vanessa Mdee kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hii ni chachu kwa wasanii wa muziki hapa Tanzania ambao bado hawaamini kuwa album inauza kwa soko letu hapa nchini.

Source: bongo5.com

Leave your comment