TANZANIA: Diamond Asogeza Mbele Tarehe ya Kuachia Album Yake ‘A Boy From Tandale’

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesogeza mbele tarehe ya kuachia album yake ya kwanza ya ‘A Boy From Tandale’.

Album hiyo ambayo awali ilitangazwa kuachiwa tarehe 23 Februari mwaka huu imesogezwa mbele hadi tarehe 7 Machi 2018.

Uongozi umeeleza kuwa sababu kubwa ya kusogeza tarehe mbele ni kupisha zoezi la utambulisho na kusimamia kazi za msanii mpya wa WCB, Mbosso ambaye ametambulishwa wikiendi iliyopita.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news