TANZANIA: Sipo Tayari Kumtangaza Mpenzi Wangu – Barnaba

Msanii wa Bongo Flava, Barnaba amesema kwa sasa hayupo tayari kumtangaza mpenzi wake.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Mapenzi Jeneza’ amesema hayo katika mahojiano na Dj Show ya Radio One na kusisistiza kuwa hata hivyo kwa sasa yupo single.

Barnaba amelazimika kusema hayo baada ya kufululiza kuposti picha za mrembo fulani katika mtandao wa Instagram bila kutolea maelezo yoyote.

“Siwezi kuzungumzia hayo acha tuone ni kitu gani kinajiri, ni kweli mimi siyo mtu wa skendo na niwaambie mashabiki sipendi stori mbaya wala sitaki kutafsirika vibaya, the good news is hakuna kibaya katika zile post zangu na sijatangaza kama ni mpenzi au la,” amesema Barnaba.

“Sipo tayari kumtangaza mpenzi wangu na sipo tayari kumsema mwanamke wangu na nipo single narudia kusem tena,” amesisitiza.

Source: bongo5.com

Leave your comment