TANZANIA: Enika, Farida, Stara Thomas na Makamua Wampa ‘Upweke’ Dayna Nyange

Msanii wa Bongo Flava Dayna Nyange ametaja orodha ya wasanii wa zamani ambao anatamani kuwasikia tena katika muziki. 

Hitmaker huyo wa Komela ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Chovya’ amewatajawa wasanii hao kuwa ni Enika, Farida, Stara Thomas na Makamua.

“Wapo wengi kwa haraka haraka kuna Makamua alikuwa akiimba vizuri, Stara Thomas nilikuwa napenda ile sauti yake nzito lakini unaweza ukawa unafeel,” Dayna ameiambia Bongo5.

“Enika na Farida ni wasanii waliokuwa wakiimba vizuri na nilikuwa nawasikia nikawanajiuliza wao wanawezaje kipindi hicho narap huniambii kitu na nilikuwa nashagaa wanawezaje kuimba hivi,” ameongeza.

Pia amesema kupotea kwa wasanii hao si kwamba wameshindwa muziki bali ni kubadilika kwa mtindo wa maisha, iwe kwenye muziki au kwao binafsi.

 Source: bongo5.com

 

 

Leave your comment