TANZANIA: Barnaba Atangaza Ujio wa Albamu Yenye Ngoma Kumi

Baada ya msanii kutoka TMK, Chege kuweka wazi mipango ya kuachia albamu yake ya ‘Run Town’ wiki hii, naye Barnaba Classic ametangaza kuachia albamu yake.

Akipiga stori katika The Playlist ya Times Fm, mkali huyo  amesema kuwa baada ya  kushindikana kuachia albamu  hiyo hapo mwanzoni kutokana na matatizo aliyopata ila sasa ana mpango wa kuachia albamu hiyo yenye ngoma kumi hivi karibuni.

“Mimi ni muimbaji nimetamani kuiona albamu yangu ikienda sokoni, i wish watu wasikie albamu yangu ambayo inakuja hivi karibuni,” amesma msanii huyo baada ya kusikiliza nyimbo zake mbili ‘Tunafanana’ na ‘Loverboy’ na kuongeza kuwa “baada ya kuzikiliza nyimbo hizi mbili naona yani kama zimebeba nyimbo 100 ukiachia zile nane zilizo bakia.”

Pia msanii huyo akasisitiza kuwa jina la albamu yake  itaiwa ‘Eight eight’ (8/8) sawa na siku yake aliyozaliwa na akaeleza kuwa  alipanga itoke albamu hii siku nyingi ila kutokana na matatizo aliyopata ya kuibiwa ikacheleweshwa hivyo kwa sasa  wana kaa na menejimenti kupanga mipango mizuri zaidi ya kuitoa.

Source: bongo5.com

Leave your comment