A-DANNY KUACHIA NYIMBO MBILI KWA MPIGO

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,A-Danny amesema atatambulisha nyimbo zake mbili mpya kwa pamoja.Msanii huyu ambaye ni mchanga katika tasnia hii ya muziki,amesema sababu ya kuachia nyimbo hizo mbili kwa wakati mmoja ni kuweza kuwapa mashabiki wa muziki huu radha mpya kwa haraka zaidi,kwani anasema tangu alipo saini mkataba na label ya FLEXIBLE BROTHERS,amejuwa akirekodi nyimbo nyingi tu katika studio za flexible music,so ana idadi ya nyimbo nyingi sana na haoni sababu ya kuendelea kukaa nazo tu,na amesema atakuwa akifanya hivyo kila atakapokuwa anaachia nyimbo.
Uongozi wa label ya FLEXIBLE BROTHERS unaomsimamia msanii huyu umesema kwa sasa wapo katika maandalizi ya kufanya video za nyimbo hizo.

Leave your comment