TANZANIA: Q Chief Amsihi TID

Msanii Q Chief amefunguka na kusema yeye hana muda wa kumjibu TID na kudai saizi yeye anaona ni muda wa kujipanga kwa ajili ya kazi zake na maisha yake kwani TID si mtu ambaye anaweza kuwa wa aina yake.

Q Chief amesema hayo leo kwenye kipindi cha Planet Bongo kufuatia TID siku ya Ijumaa kupitia Friday Night Live kusema yeye hamtambui Q Chief na wala hamjui ndipo Q Chief aliposema hana muda ya kuanza kuhangaika kujibizana na TID. 

"Mimi na Mnyama hatuna tofauti watu wanabidi waelewe kuwa Q Chief inabidi ajikite na kazi zake mimi nikichukua muda mwingine kumjibu TID maana yake ni kwamba natumia muda mwingi na nguvu kubwa kumzungumzia mtu ambaye anafanya kazi zake. Mimi naheshimu nini anazungumza na kile anafanya lakini Q Chief ni mtu aliyekuwa, mtu mwenye majukumu ambaye sasa anajaribu kutafuta njia ya kufanya vitu vizuri kwa hiyo sina muda wa kubishana na watu ambao najaribu kuwaweka kwenye viatu vyangu sioni kama vinawatosha" alisema Q Chief.

Mbali na hilo Q Chief alisema anamuheshimu TID pamoja na muziki wake ila akamtaka awe na heshima kwa watu ambao wamemfanya yeye ajione ni kati ya watu wakubwa Tanzania 

Msikilize hapa Q Chief akifunguka zaidi:

 
Source: eatv.tv
 
 

 

Leave your comment