TANZANIA: Barakah The Prince Ajitoa RockStar4000

Msanii wa Bongo Flava, Barakah The Prince amejitoa chini ya usimamizi wa RockStar4000.

Muimbaji huyo amesema kuondoka kwake hakuhusiani na Alikiba ambaye ni mmoja kati ya director wa label hiyo bali ni baadhi ya mambo na uongozi wa RockStar4000 hayajakaa sawa.

“Sipo chini ya RockStar kwa sababau mimi ndio bosi wa muziki wangu, halafu mwisho wa siku mimi ndio nafanya kazi kwa hiyo kukiwa na vitu ambavyo haviko sawa kwa upande wangu naweza kutoa kauli ya mwisho kwa hiyo sipo RockStar kuna vitu ambavyo havipo sawa,” ameiambia XXL ya Clouds Fm.

Alipoulizwa kama kujitoa kwake kuna uhusiano na Alikiba kuwa miongoni mwa wamiliki wa label hiyo, Baraka amesema, “Hapana hili haliwezi kuwa tatizo kwa sababu Alikiba ni director wa RockStar mimi nijitoe, hapana!!, sema kuna vitu havipo sawa kati yangu na uongozi wa RockStar wao kama wao ambao nilisaini nao, mimi sijasaini mkataba na Alikiba. Kwa hiyo ukiona chochote cha Barakah ipo under Barakah”.

Source: bongo5.com

Leave your comment