TANZANIA: Vanessa Mdee Aeleza Video Yake Kufanana na ‘Energy’ ya Keri Hilson

Vanessa Mdee amefunguka video yake ya wimbo wa ‘Kisela’ kutajwa kufanana na ile ya Keri Hilson ‘Energy’ iliyotoka miaka takribani saba iliyopita.

Akiongea na kipindi cha The Playlist cha Times FM, muimbaji huyo amesema, jap amekuwa akivutiwa sana na wimbo huo lakini kwenye uandishi wa script ya video ya wimbo wake huo mpya hajashiriki kuandika hata kidogo, aliyehusika zaidi ni director wa video hiyo Clarence Peter.

“To be honest mimi napenda sana huo wimbo, I love the video, I love Keri Hilson but I did,’t think about that video at all. In fact hii script mimi sikuandika kabisa, usually na play part kwenye script write lakini sikuandika kabisa, aliandika Clarence, alinitumia the hall script. When I was doing I said okay great but now when people started to refer nikasema duuh! Maybe but there’s no original concept,” amesema Vee Money.


Picha ya video ya wimbo wa Keri Hilson ‘Energy’ iuliyotoka mwaka 2009

Msanii huyo ameongeza pia video hiyo inafanana na video nyingine mbili ikiwemo moja ya Uganda na kuna nyingine ya Bollywood.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news