TANZANIA: Vanessa Mdee Kamtambulisha Msanii Mpya Kwenye Label Yake

Vanessa Mdee ni miongoni mwa wasanii wenye labels hapa Tanzania ama kampuni ya kusimamia kazi za wasanii inayojulikana kama Mdee Music ambayo ndani yake alikuwepo yeye na mdogo wake ambaye ni Mimi Mars.

Leo June10 kupitia kipindi cha XXL ya Clouds FM V Money amemtambulisha msanii mwingine mpya ambaye ameongezeka kwenye label hiyo ya Mdee Music. Vanessa alimtambulisha msanii huyo kama Brian Simba na kusema kuwa ni msaniii wa tofauti sana ana rap kipekee na anamuona kwenye level za Kendric Lamar.

View image on Twitter
 
 
Source: millardayo.com

Leave your comment

Other news