TANZANIA: Mansu-Li Atia Neno Vita ya Michano Kati ya Wakazi na Godzilla

Msanii wa muziki wa hip hop nchini, Mansu-Li ameamua kutia neno katika vita ya mistari inayoendelea kati ya Wakazi na Godzilla.

Rapper huyo ambaye kwa sasa anasikika na ngoma yake mpya ‘Hip Hop’, amesema mvutano huo utakuwa ni mzuri endapo utaishia katika kuchanana kwenye nyimbo tu lakini itakuwa vibaya iwapo mmoja wapo atachukulia hilo suala kibinafsi na kulipeleka nje ya muziki kitu ambacho kitakuwa siyo kizuri.

“Hiyo hatusemi ni chuki, bali ni game, mbaya kama tutachukulia person. Hiyo ndio mbaya zaidi, labda mimi nakutana na Nay hatuongei kwa sababu mstari wake fulani ulinihusu lakini kwa mtu ambaye anajua game huwezi kuchukia,” Mansu-Li amekiambia kipindi cha Daladala Beat ya Magic FM.

“Mbona time ile Madee amesema Hip Hop haiuzi, lakini Madee ni mchizi ambaye sometime naweza nikampigia Madee vipi, fresh, nipo pande za Manzese tunazinguana, tunacheka fresh kwa nini nisingekichukulia person kwa vile kitu ninachokifanya Madee anakizarau lakini mimi nilichukulia ni game na nimawazo yake,” ameongeza.

Mansu-Li amesisitiza kwa kusema, “Unasikiliza yale mashairi yake unaona na mimi nakuja vipi, ni kama tunavyokuwa kwenye freestyle battle. Mimi nasikiliza kama ulivyonichana, najua umenichana hivi na mimi nije vipi, labda mimi kuna vitu vyako navijua au Wickness zako na mimi nakushambulia.”

Source: bongo5.com

Leave your comment