TANZANIA: Bill Nass Afunguka Kuhusu Kilichopo Kati Yake na Godzilla

Staa anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongofleva Billnas amekana taarifa zinazodai kuwa ana tofauti na staa mwingine wa Bongofleva Godzilla akisema hana tatizo naye na ameshakutana naye mara nyingi ingawa kuna watu wanadai hivyo.

Kutokana na hali hiyo Billnas amekiri kupigiwa simu na Godzilla akimpa ushauri na kumtia moyo kwa kile anachokifanya akisema pia kuwa uhusiano wao uko vizuri na mara nyingi ‘King Zilla’ amekuwa akisikiliza nyimbo zake.

Mbali na hayo, Billnas pia amegusia inayoitwa vita ya maneno kati ya Godzilla na Wakazi akisema hawezi kuingilia kwa sababu inawezekana wawili hao wamepanga au wanajua wenyewe kwa kuwa mambo hayo yalishakuwepo tangu zamani.

Source: millardayo.com

Leave your comment