TANZANIA: One the Incredible na Chaba Wafunguka Kuhusu Stress Kwenye Muziki

Wasanii wa Hip Hop, One the Incredible na Chaba amechambua baadhi ya mambo ambayo yanawapa wasanii wengi msongo wa mawazo pindi wanaposhuka kimuziki. Mingoni mwa sababu walizotaja rappers hao ni baadhi ya wasanii kutokuwa na vyanzo tofauti vya mapato na kushindwa kuandaa show zao mwenyewe.

Wakizungumza katika kipindi cha Ladhaa 3600 cha E FM, Chaba amewataka wasanii kutoweka mayai yote kwenye kapu moja kwa sababu ipo siku hilo kapu likidondoka na mambo yao yataenda kombo na pengine hata kulala njaa.

“Msanii hatakiwi kutengemea sanaa tu. Unajua siku hizi kila mtu anakua msanii na wanakuwa na menejimenti zao, hivyo ushindani ni mkubwa kwa hiyo kama utategemea tu sanaa na hutafanya vitu vingine utakwama,” amesema Chaba.

“Na akili inahitaji kupumzika ndio maana unaona sasa hivi hata Jay Z hafanyi sanaa, anafanya masuala ya kifamilia  anapumzisha hata ile akili, siku amerudi na albamu yake utaniambia,” ameongeza.

 

Kwa upande wake One the Incredible amesema kila mtu ana investment yake kwenye kitu fulani kutokana na vile yeye anavyoamini ile investment yake na return yake kwa kile anachokifanya.

“Kwangu mimi muziki ni platform ambayo inaweza kunipeleka katika biashara nyingine nyingi na kubwa zaidi,  so ningependa focus hiyo iwe na professionalism hata nikisema naenda kupick tenda fulani wanaona hata jamaa anachokifanya ni katika level fulani inayoeleweka. Katika vitu ambavyo nimejifunza katika hii industry ya sanaa hakuna mtu ambaye atakuja kukufanyia kitu chako. Ukiangalia ni wasanii wanaoandaa event zao wenywewe hawafiki watano,” amesema One.

“Ndani ya Tamaduni moja ya sababu kuwa na ule muunganiko ni kwa sababu tunaweza kufanya vitu vyetu wenyewe. Tunaweza tukafika Mwanza tukachukua ukumbi tukaweka bidhaa zetu zikauzwa, tukafanya show yetu mwisho wa siku mnajipigia hesabu. Mtu kama Jay Z asingekuwa alipo kama asingekuwa anafanya tour zake mwenywe,” amesistiza One.

Hapo jana kulikuwa na mvutano katika mtandao wa twitter kati wa wasanii wawili wa Hip Hop, Wakazi na Godzilla, katika kutupiana maneno ilifika mahali Wakazi akadai rapper mwenzake anapewa stress na Bill Nass. Hiyo ikiwa ni mara nyigine  Godzilla kuambia hivyo katika mtandao huo baada ya mtangazaji Diva kufanya hivyo.

Source: bongo5.com

Leave your comment