TANZANIA: Natamani Mwaka Huu Ndio Ningeanza Muziki - Bill Nass

Rapa Bill Nass amefunguka na kusema angetamani mwaka ndio angeanza muziki kwa sababu ndio anamaliza chuo kwani wakati anafanya muziki na kusoma kumemfanya kupoteza fedha nyingi.

Bill Nass ameimbia show ya E News kuwa wakati ametoa wimbo wa Chafu Pozi alipata dili nyingi sana ila masomo yakambana kuzifanya ila ni kitu ambacho hawezi kukijutia kwa sababu bado anafanya vizuri kwenye muziki.

“Ujue kufanya muziki na Chuo nimepoteza hela nyingi sana watu wengine hawawezi kujua, nishakataa show nyingi sana, nishaacha kwenda matamasha kibao, vitu vingi sana vya kimuziki vilinipita. Kipindi Chafu Pozi ina wiki nilikuwa napata dili nyingi ambazo unajua hela yake ilikua nzuri.

“Ningekuwa najua ningemaliza mwaka wangu wa tatu ndio nikaanza muziki alafu zile (hela) ndio niwe ninakutana nazo hapa lakini sio mbaya namshukuru Mungu hiyo ndio imenifanya nimekuwa BilNass watu wengi wananipenda huwezi jua mbeleni kuna nini, kwa hiyo tunaendelea kupambana na uzuri tunaendelea kufanya vizuri,” ameeleza Bill Nas.

Rapa huyo ameongeza kuwa wimbo wa Mazoea ni mkubwa na imetengeneza hela nyingi sana lakini kile anachokipoteza lazima akiwazie kwa sababu kuna fedha nyingi aliziacha kwa sababu ya shule.

“Basi hii shule izirudishe, kwa sababu mazoea ina bajeti yake imetoka na imekuwa kubwa na imerejesha bajeti yake na faida, kuna ambayo ilitengwa kwenye Chafu Pozi ikarudi na faida lakini kuna faida nyingine ambayo tunasema opportunity cost, kuna hela nyingine ilikuwepo tungeipata pia,” ameeleza Bill Nass.

Source: bongo5.com

Leave your comment