TANZANIA: Stamina Aibuka Kumtetea Vanessa

Rappa Stamina amekanusha vikali tuhuma za kushindwana na mwanamuziki Vanessa Mdee kurekodi wimbo walioshirikiana kwa madai ya kutofautiana juu ya 'director' wa kufanya naye kazi na kusema kuwa wimbo wao haujakamilika watu wasimchafue msanii huyo.

Mbele ya kamera za eNewz Stamina amefunguka na kudai habari za kushindwana na Vanessa Mdee kuhusu 'director' kati ya Hanscana au mwingine ndio afanye kazi yao  ni za uzushi kwani hawajawahi kuongelea suala la ku'shoot' video kwa kuwa wimbo wenyewe haujakamilika bado.

"Watu wasimsingizie Vanessa, hajawahi kunipa tabu na wala hatujawahi kuongea kuhusu suala la ku 'shoot video'  kwa kuwa wimbo wenyewe bado upo studio. Vanessa kuna vipande hajakamilisha kuviingiza na wimbo una makosa ya kurekebisha siku tukiumaliza tuu tutautoa hadharani. Siyo kweli kama nimetoa wimbo na Maua kwa sababu nimeshindwana na Vanessa Mdee"- alisema Stamina.

Habari zinadai kuwa Stamina na Vanesa walishindwa kuachia video yao ambayo kila mmoja alikuwa na uchaguzi wa director wa kufanya naye kazi kitu ambacho  kilimpelekea kuachia kazi mpya na Mwanadada Maua Sama inayokwenda kwa jina la  'Love Me" japokuwa Stamina amedai siyo kweli.

Sourse: eatv.tv

Leave your comment

Top stories

More News