TANZANIA: Kila Mwezi Nitatoa Ngoma na Video – Stamina

Msanii wa miondoko ya Hip Hop kutoka Morogoro, Stamina amesema albamu yake ya pili imekamilika hivyo ataanza kutoa wimbo kila mwezi kutoka kwenye albam hiyo.

Stamina

Stamina amesema ukimya wake kwenye game kabla ya kutoa wimbo mpya aliomshirikisha Maua Sama ‘Love Me’ ulisabababishwa na maandalizi ya albam hiyo pamoja na kurekebisha makosa yaliyokuwa yakijitokeza katika muziki wake.

“Nimemaliza kurekodi albamu yangu ya pili ambayo ina nyimbo 15 na tunairelease next month, kwa hiyo unaweza ukaona ukimya wangu ulikuwa ni seriousness na sasa hivi tunavunja ule ukimya na kila mwezi nakuwa naleta ngoma, yaani audio na video nataka niwaonyeshe watu ukimya wangu ulikuwa na manufaa zaidi kuliko hata ningekuwa naendelea kutoa nyimbo,” Stamina ameiambia Show ya Daladala Beat na kuongeza.

“Nikasema najipa time ya changes unajua ukijua pale ulipokosea ukapafanyia marekebisho ni maendeleo, kwa hiyo nikajiweka pembeni nikaanza kuandaa magoma, kwa hiyo this time around nataka kuwaonyesha watu kuwa naweza kufanya chochote kile wanachotaka,” amesema Stamina.

Source: bongo5.com

Leave your comment