TANZANIA: Stamina Amtangaza Meneja Wake Mpya
19 May 2017
Mkali wa muziki wa Hip Hop kutoka Morogoro, Stamina, amemtangaza prodyuza Maneck kutoka AM Records kuwa ndiye meneja wake kwa sasa.
Wakati akitambulisha wimbo wake mpya ‘Love Me’ aliomshirikisha Maua Sama kwenye kipindi cha XXL, Stamina alitumia nafasi hiyo kumtangaza Maneck na kuelezea mipango yake ya kazi kwa sasa na siku zijazo.
“Ngoma yangu mpya na Maua Sama kafanya Bear chini ya Kiri Records na wala si Am Records, lakini nipo hapa na Maneck kwa sababu sasa hivi yeye ni meneja wangu. Tupo katika kampuni moja, yeye katika hiyo kampuni ni ndiye meneja, bosi yupo. Kampuni yetu inaitwa ‘Babaz Entertainment’,” amesema na kuongeza.
“Huwezi kuamini, mimi bosi wangu ni shabiki wangu kabisa ni mtu ananipenda kutoka moyoni. Mazingira tuliyokutana, akaniambia wewe basi tu napenda kazi zako, basi tuunganishe nguvu tulichonacho tufanye. Namshukuru Mungu sasa hivi kila mwezi nitakuwa nawasurprise,” amesema Stamina.
Source:bongo5.com
Leave your comment