TANZANIA: Billnass Ataja Sababu ya Wasanii Kuringa

Mzungu Mzee 'Billnass' anayesumbua na ngoma ya 'Mazoea' ameweka wazi kinachowafanya wasanii wengi waonekane wanaringa na kusema wengi wao hukumbuka mateso na manyanyaso ambayo huwa wanapitia kabla ya kutoboa lakini pia ni mbinu za kibiashara.

Billnass amefunguka hayo kwenye Planet Bongo ya EATV na kusema kuwa wasanii wengi siyo kwamba wanaringa bali huamua kukaa maisha ya mbali na wale watu kipindi walipokuwa wanatafuta misaada halafu wakawa wanawanyima, hivyo wanapotusua na wao wanakuwa hawataki mazoea.

"Mimi ni social sana ndo maana hata maneno mengi yananipata, wasanii wanaonekana wanaringa kwa sababu hawataki zile kujuana sana ndiyo kuharibiana CV so usinijue kama hauna plan B' ndo mazoea hawataki. Unajua visasi siyo vizuri lakini kuna watu wakiwa wana 'hustle' huwa wanawakariri nani na nani walinipa msaada nani alinikazia kwa hiyo akifanikiwa anaamua kuishi maisha yake binafsi ya kukaa mbali na watu wanafiki" Amesema Billnass.

Hata hivyo msanii huyo ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha CBE amedai licha ya kuwa anachukua kozi ya manunuzi (Procurement) anampango wa kuwa mfanyabiashara mkubwa na kabla ya kujiajiri atataka kuajiriwa na kufanyia kazi elimu yake.

"Nina ndoto za kuwa mfanyabiashara mkubwa, lakini elimu yangu ambayo naichukua lazima niifanyie kazi hata nikajiriwa miaka miwili inatosha kabisa ili niweze kwenda kujiajiri peke yangu kwenye biashara ninazoplan kuzifanya", alimalizia  Billnass.

 Source: eatv.tv
 

Leave your comment