TANZANIA: Belle 9 Ajitetea Kuhusu Ngoma Yake 'Kubuma'

Msanii Belle 9 amekanusha tetesi zinazosambaa kwamba 'amefulia' kwenye muziki baada ya kuachia wimbo wake  wa Mzuri na kusema hajafeli kimuziki.

Akipiga story kupitia eNewz Belle 9 amesema mesema wimbo huo wa Mzuri unaodaiwa kutofanya vizuri, aliamua kuuachia kwa ajili ya kumchangia msanii Jetman kwa kuwa alitumiwa 'biti' kwa ajili ya kuchangia mchango wa Jetman kupata pesa ya matibabu, vinginevyo asingeutoa

"Kwa kuwa Jetman aliamua kutengeneza bit na kuwauzia wasanii ili waweze kumchangia basi nikaamua kuachia nyimbo kwa ajili ya kumsaidia na hata hivyo wasanii wengi ambao walinunua biti waliachia nyimbo ila hazikusikika kwa kuwa hazikuwa  kubwa". Alisema Belle 9 na kusisitiza  "Wimbo wa Mzuri nimeuimba kwa ajili ya kumchangia Jetman na siyo project yangu mpya"

Akimuelezea Jetman, Belle 9 amesema Jetman alikuwa ni msanii wa bongo fleva ni muandaaji wa 'biti' pia alishawahi kuwa mbunifu wa mavazi na alishawahi kuwavalisha Weusi.

Source: eatv.tv

Leave your comment