TANZANIA: Kilichofanya TID Amuite Jide 'Genious'

Akiwa anaachia ngoma yake impya yenye jina la 'Woman' TID amesema wimbo wake huo aliutengeneza tangu mwaka uliopita hivyo hakuwa anajua kama mwana dada huyo ana albam inayofanana na jina la track yake.

"Jide is a woman but mimi ni mwanaume ninayeimba kuhusu mwanamke. Huwezi amini kama mimi albamu yangu pia inaitwa Woman na kama Jide albamu yake inaitwa woman jua mimi ni hatari sana. Sasa kama mimi nina uwezo wa kufikiria kama Lady Jaydee basi mimi nitakuwa genious kufikiria kama lady Jaydee si kitu cha kitoto" Alisema TID

Katika hatua nyingine TID amesema video yake ya Woman ni kazi ambayo imekuja kufanya mapinduzi kwenye kazi zake zote kwa sababu imegharimu dolla 12,000 (zaidi ya shilingi milioni 25 za Tanzania) na imefanyika nchini Afrika Kusini

Pamoja na hayo ameongeza kuwa ule ushirikiano aliokuwa anaupata mwanzo kutoka kwa wale aliowaita kaka zake umepotea baada ya kukiri kuwa yeye ni mtumiaji wa madawa ya kulevya na anataka kuacha.

"Mwanzo nilikuwa natoa milioni mbili lakini kwa sababu nataka quality na nimefanya peke yangu, To me brothers wote wamenitenga kwa sababu niliconfess natumia drugs, hawanisapoti sijui walitaka nipotee" TID alihoji.

Source: eatv.com

Leave your comment