TANZANIA: Azma Mponda Atikisa Zaidi Kenya Kuliko Bongo

Msanii Azma Mponda kutoka Mbeya amefunguka baada ya kukosa soko la muziki Bongo anadai lugha ya Kiswahili ndiyo iliyompatia nafasi nchini Kenya.

 

Amesema Kenya walimpokea kwa namna ya tofauti hadi kupelekea wasanii wakubwa wa nchi hiyo kuanza kuomba kolabo hali iliyomfanya kujihisi muziki wake una thamani kuliko alivyofikiri.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Mponda amedai kwamba alitumia muda mrefu kutafuta soko la muziki nchini hakuona kama anathaminika lakini Kenya walimpokea kama mfalme hadi kumfanya Nameless pamoja Khaligraph Jones kutaka kufanya naye kazi.

"Nilipomaliza chuo niliendelea na mishe za kutafuta channel za muziki lakini naona mambo yakawa magumu kiasi kwamba nikaanza kukata tamaa nikiwaangalia niliosoma nao wameshanizidi, nikaamua kwenda Kenya lakini cha ajabu nyimbo zangu kule zilikuwa kubwa sana na msanii wa kwanza kufanya naye kazi akawa ni Khaligraphs nikaona tayari nimeshapenya wakati huo huo Namless naye akawa anataka kollabo". Amesema Azma

Katika hatua nyingine Mponda ameongeza kuwa watu walishaanza kumfikiria kuwa ni mkenya ndio sababu akaamua kuachia kazi aliyowashirikisha Izzo Biznez , Sugu pamoja na Abbela Music inayotambulika kama 'Garagasha" ili watu  wamtambue kama mtanzania kabla hajaanza kutoa kolabo alizoshirikiana na wsanii kutoka Kenya, USA pamoja na UK.

Source: eatv.tv

Leave your comment