TANZANIA: One The Incredible Aeleza Kwa Nini Ngoma Yake Mpya My City ni ‘Trap’

One The Incredible amejizolea heshima kubwa kwa uandishi mahiri wa hip hop pamoja na kusimamia misingi ya muziki huo.

Hata hivyo, tofauti na wengi wanavyomjua, One ni mtu aliye ‘flexible’ kufanya muziki wa aina mbalimbali na ndio maana ngoma yake mpya, My City ina vionjo vya trap, muziki ambao baadhi ya wasanii wa hip hop hawataki hata kuusikia.

One ameiambia Bongo5 kuwa lengo la kufanya trap ni kuhakikisha anasogea mbele zaidi kisanaa kwa kukuza idadi ya mashabiki wake. Amesema kama angeendelea kuliridhisha kundi lile lile la mashabiki wake bila kuongeza wengine, hawezi kukua kisanii.

Kingine amedai amesema anajitahidi pia kuchanganya sound mpya ya hip hop kwenye muziki wake ili kwendana na wakati. Kwa upande mwingine One amedai kuwa hata wakati yuko shuleni, alikuwa akitumia zaidi beats za trap na hadi ametoa My City, washkaji wake aliosoma nao wamempigia simu kumwambia kuwa wamemmiss akirap katika mahadhi hayo.

Source: bongo5.com

Leave your comment