TANZANIA: Nitafanya kazi na Jay Z - Rosa Ree

Rapa Rosa Ree kutoka lebo ya The Industry inayosimamiwa na kundi la Navykenzo, amesema bado anandoto siku moja ya kufanya kazi na rapa mkongwe anayefanya vizuri Marekani na ulimwenguni kwa ujumla Jay Z.

Akizungumza jana kwenye kipindi cha Friday Night Live cha EATV, Rosa Ree alisema bado ndoto zake za kutaka kufanya Kolabo na msanii Jay Z hazijafutika kichwani kwake na bado anaamini ipo siku itatokea huku akisema kwa nyumbani bado hajachagua msanii gani wa kumshirikisha katika nyimbo zake ingawa kwa wasanii wa bendi Christian Bella huwa anamkosha zaidi.

"Ndoto ya kufanya kazi na Jay Z bado ipo ni kitu ambacho naamini nitakifanya muda ukiwadia, kwa nyumbani sijaamua bado nani wa kufanya nae kazi kwa sababu wapo wengi sana lakini kwa upande wa bendi Christian Bella sauti yake inanikoshaga sana maana ana sauti flani nzuri sana".- alisema Rosa Ree.

Source: eatv.tv

 

Leave your comment