TANZANIA: Wasanii Watano Anaowakubali Lady Jaydee

Msanii mkongwe katika muziki wa bongo fleva Lady Jaydee amewataja wasanii watano katika muziki wa bongo fleva ambao anawakubali zaidi kutokana na kazi zao na uwezo wao.

Lady Jaydee akiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio aliwataja wasanii anaowakubali na wanaomfurahisha kutokana na kazi zao na uimbaji wao  kuwa ni pamoja na Ben Pol, Ruby, Vanessa Mdee, Shaa pamoja na Mr. Blue

Mbali na hilo Lady Jaydee alisema kuwa soko la albam kwa sasa limekufa lakini hiyo hamtamzuia yeye kutoa albam yake na kwamba anatoa albam ili kulinda heshima yake na kuweka heshima kwa mashabiki ambao wanapenda muziki wake. 

"Soko la albam limekufa kabisa ila nachofanya ni kuweka ile heshima na kuwapa heshima wale mashabiki wangu wanaopenda muziki wangu, hivyo sitegemei kupata faida sana. Pia nitauza albam yangu ya 'Women' online, kwenye matamasha mbalimbali na nitakakokuwa nakwenda kufanya show nitauza albam yangu" alisema Lady Jaydee.

Source: eatv.tv

 

Leave your comment

Top stories

More News