TANZANIA: Chemical amtosa rasmi Stereo

 

Rapa wa kike bongo Chemical ameamua kufunguka ya moyoni na kuweka wazi kuwa sasa hawezi kuwa na mahusiano na rapa Stereo kwani anaona rapa huyo kama hayupo 'serious'


Siku Stereo alipokutamishwa na Chemical LIVE kwenye kipindi cha Friday Night Live cha EATV. Chemical amesema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kudai anaona Stereo hamaanishi anachokisema na kuwa hayuko 'serious' kwenye jambo hilo ambalo alikuwa akiliimba sana kupitia vyombo vya habari, kwa sababu hajaona hizo jitihada zake. 

"Mimi nilisema kama kweli Stereo yupo serious anitafute lakini hajanitafuta, off course amenitafuta kama kunitafuta lakini siyo ile serious, unajua nikimkubali haraka anaweza kunichukulia poa, ila naomba nisema tu Stereo saizi atafute mtu mwingine kama Mungu kapanga tutakutana na kama hajapanga basi tena, pleasee Stereo" alisisitiza Chemical. Mbali na hilo, rapa huyo amesema mpaka sasa amefanya kazi na Fid Q pamoja na Mr. Blue na kusema kuwa ni kazi nzuri sana hizo ambazo anasubiri muda wake ufike tu ili aanze kuachia kazi hizo.

Leave your comment