TANZANIA: Belle 9 nae achukua vionjo vya Saida Karoli

 

 

Baada ya Diamond na Darassa kuchukua baadhi ya vionjo katika nyimbo za Saida Karoli sasa ni zamu ya Belle 9 ambaye na yeye ametumia baadhi ya vionjo vya moja ya nyimbo zake kutengenezea wimbo wake 'GIVE IT TO ME'.

 Alipozungumza na eNewz weekend hii wakati akizindua video ya wimbo huo alisema kuwa wimbo tayari alikuwa ameshaufanya toka kitambo kwa kutumia vionjo hivyo katika wimbo wa Saida Karoli na sio kwamba amekopi au amefanya kwa sababu watu wengine wamefanya.

“Mimi huo wimbo nilikuwa nimeufanya toka muda mrefu na siyo kwamba nimeona watu wametoa ndiyo nimetoa na wazo hilo nilikuwa nalo toka kitambo sana pia kuhusu G Nako kuimba sehemu ndogo ni kwa sababu tulikuwa tumegawana mashairi na siyo kama nimembania” Amesema Belle 9

 

 

Leave your comment