TANZANIA: Inanishangaza sana kwanini wanawake kwa wanawake hatusapotiani - Ruby

 

Ruby amefunguka kwa kudai kuwa wasanii wengi wa kike kwenye muziki wamekuwa ni wabinafsi.
Muimbaji huyo mwenye sauti ya dhahabu, amemuambia mtangazaji wa kipindi cha Playlist cha Times FM, Lil Ommy kuwa huenda kungekuwa na wasanii wengi wa kike kwenye Bongo Fleva kama wangekuwa wanashirikiana kwa kufanya kazi kwa pamoja.


“Mimi hainiumi ila inanishangaza sana kwanini wanawake kwa wanawake hatusapotiani, mbona wanaume kwa wanaume wanafanya muziki wanafanya vitu vingi pamoja. Ni kitu cha ukweli kabisa kwenye industry wanawake hatufanyi kolabo wanawake kwa wanawake, ni kitu ambacho si kizuri kwa sababu huenda tungekuwa na wasanii wengi wa kike kwenye muziki,” amesema Ruby.

Ruby ameongeza kuwa msanii unatakiwa uwe mnyeyekevu kwa kila mtu lakini uangalie ni wakati gani unatakiwa kufanya hivyo.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment