TANZANIA: Christian Bella atumbuiza Ikulu jana
5 October 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Jumanne hii alimwandalia dhifa ya Taifa, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila wakiagana na viongozi wastaafu Ikulu jijini Dar es salaam
Shughuli hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkali wa masauti Christian Bella alikuwa mmoja kati ya wasanii ambao walialikwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kusherehesha shughuli hiyo. Angalia picha.
Mama Janeth Magufuli akimtuza mwanamuziki Christian Bella kwa kutumbuiza wimbo maarufu wa “Nani kama Mama” kwenye dhifa hiyo
Msanii mkongwe Zahir Ally Zorro alikuwepo kutoa burudani
Spika Mstaafu Mhe Anne makinda akimtuza mwanamuziki Christian Bella kwa kutumbuiza wimbo maarufu wa “Nani kama Mama” kwenye dhifa hiyo
Mama Salma Kikwete akimtuza mwanamuziki Christian Bella kwa kutumbuiza wimbo maarufu wa “Nani kama Mama” kwenye dhifa hiyo
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akimtuza mwanamuziki Christian Bella kwa kutumbuiza wimbo maarufu wa “Nani kama Mama” kwenye dhifa hiyo
Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz
Leave your comment