TANZANIA: Koffi Olomide anyimwa dhamana, asota rumande

 

 

Mwanamuziki maarufu Koffi Olomide amenyimwa dhamana ya kuachiliwa huru kulingana na wakili wake. Muimbaji huyo baada ya kupandishwa mahakamani alikanusha tuhuma zinazo mkabili huku jaji alikataa ombi lake la kuachiliwa kwa dhamana.

Siku ya Jumatatu, maafisa wa polisi walimkamata Olomide mwenye umri wa miaka 60 nyumbani kwake katika makaazi ya Kinshasa baada ya kupatikana katika kamera akimpiga teke mmoja wa wanenguaji wake katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini nairobi. Alirejeshwa nchini DRC kutoka Kenya kufuatia kisa hicho cha Ijumaa.

Hatua hiyo ilisababisha kufutiliwa mbali kwa tamasha lake nchini Kenya na Zambia.

 

Source: BBC

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment