TANZANIA: Baada ya Sony Music , AliKiba apata dili la Jamie Oliver Food Foundation

 

Huu ni mwaka wa Alikiba. Baada ya kusaini mkataba mnono na Sony Music itakayomshuhudia akienda rasmi kimataifa, staa huyo amepewa dili jingine la kufanya kazi na taasisi ya Jamie Oliver Food Foundation.

Trace Urban wameshare habari hiyo kwenye Twitter. “This is .@OfficialAlikiba’s year! He has a dope partnership w/the #JamieOliverFoundation too.”

 

Taasisi hiyo ya kimataifa inajihusisha na masuala ya chakula na upishi. “Access to good, fresh, real food and the basic skills to cook it has the power to transform lives, and that is what the Jamie Oliver Food Foundation is all about,” imeandika kwenye tovuti yake.

 Taasisi hiyo inafanya kazi Uingereza, Marekani Australia na hutoa mafunzo mbalimbali kuhusu chakula. “Our food education programmes in schools, communities and with groups of vulnerable young adults teach people about food, where it comes from, how it affects their bodies and how to cook it.”

 

 

Taasisi hiyo ilianzishwa na mpishi maarufu wa Uingereza, James Trevor Oliver

Katika hatua nyingine mkataba wa Alikiba na Sony utamwezesha kufanya collabo na msanii wa Marekani aliye chini ya label hiyo pia.

“@SonyMusicAfrica will have USA/East Africa collaboration for @OfficialAlikiba with other #Sony artists,” wametweet Trace.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

Chanzo: Bongo5

 

Leave your comment