TANZANIA: Ommy Dimpoz alinisumbua sana - AliKiba

 

Akiongea na East Africa Radio Alikiba alidai kuwa ilimchukua takribani mwezi mmoja kama si miwili ili kufanya kazi hiyo na Ommy Dimpoz kwani anadai kila alipomuahidi kwenda studio mambo yaliingiliana na kujikuta inakwenda zaidi ya miezi miwili ndipo alipopata nafasi na kwenda studio kukamilisha Collabo hiyo.


"Ommy Dimpoz alikuja akaniambia Kaka kuna wimbo fulani nataka tufanye, mimi nikamuuliza wewe si unaimba kwenye band? akaniambia ni kweli ila kwa sasa nataka kutoka mwenyewe nikamwambia sawa. Nikamuuliza wimbo huo umefanya wapi akasema kwa KGT nikamwambia pale ni nyumbani kwangu, hivyo nikapata nafasi kuisikiliza kazi ile na kumwambia wimbo huu unahitaji vitu vya ziada. lakini ilinichukua zaidi ya mwezi kama si miezi miwili kwenda studio sababu mambo yalikuwa yanagingiliana lakini alikuwa akizidi kunisumbua si kwa nia mbaya au kwa ubaya ni vile mambo yangu yalikuwa mengi na yalikuwa yanaingiliana ila nakumbuka majibu yangu yalikuwa ya matumaini kwake" alisema Alikiba


Mbali na hilo Alikiba alitoa siri yeye kufanya kazi ambazo zinapendeka na mashabiki ni kwa sababu mara nyingi anapofanya kazi huwa anaangalia mashabiki zaidi na si kuangalia yeye ile kazi anaionaje, pia alisema katika ufanyaji kazi huwa anafanya kazi kwa kufuata hisia zake na si kukurupuka tu studio na kufanya kazi.


"Unajua mimi siku zote huwa nafanya kazi kwa 'feelings' hata nikiwa studio naweza nikakaa tu mpaka hisia zinijie ili nikifanya pale kazi watu waweze kuielewa" aliongeza Alikiba

Leave your comment