TANZANIA: AliKiba -“Siwezi kuoa mama wa watoto wangu yeyote niliyezaa nae”.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba amesikikika akisema kuwa, hataweza kumuoa mwanamke yeyote aliyewahi kuzaa nae.

Msanii huyo wa bongo fleva amekiambia kituo cha Radio Free Africa (RFA) kupitia kipindi chacke cha chill and sky na kusema kuwa,” Huwezi kumuoa mtu kama hamuelewani. Nia yangu ilikuwa kustick na kila mama wa mmoja toka nilipoanza, lakini mambo yanaenda tofauti, huenda mnagombana au anapata mtu mwingine”.

Msanii huyo ambaye ni baba wa watoto watatu, wakike wawili wa kike Amiya na Chammy Kiba pamoja na mmoja wa kiume Sameer Kiba ambaye kila mmoja ana mama yake.

Leave your comment