EXCLUSIVE (TANZANIA) – 2015 Nimepata pesa nyingi kwenye muziki kuliko mwaka mwingine – Mr Blue
14 December 2015
Msanii Herry Samir maarufu kama Mr Blue amesema mwaka 2015 muziki umemuingizia pesa nyingi kuliko mwaka mwingine.
Ambapo pia kwa mwaka huu mbali na kuingiza pesa nyingi mwanamuziki huyo pia amebahatika kuongeza familia yake, kwa kupata mtoto mwingine wa kike na kwa sasa jumla ana watoto wawili (wakike na wakiume).
Pamoja na kusema kuwa amepata pesa nyingi lakini hakutaja ni kiasi gani, Mr Blue amesema kutokana na show za mwaka huu ndizo zimefanya kuvunja rekodi ya miaka yote iliyopita.
Vyanzo vya mafanikio hayo ni show, mauzo ya nyimbo mitandaoni, caller tune na vitu vinavyohusiana na muziki.
Mr Blue alimaliza mwaka jana kwa kufanya show kali ya Fiesta jijini Dar es salaam na mikoani kitu ambacho kilionyesha bado kuna mashabiki wengi wanamkubali na ku-miss show zake.
Pichani; Watoto wa Mr Blue
Source: Millardayo.com
Leave your comment