EXCLUSIVE (TANZANIA) – Toka usanii hadi ufugaji wa kuku – Mr Nice
11 December 2015
Mwanamuziki Mr Nice kwa sasa hategemei tena muziki peke ake bali ufugaji wa kuku. Ambapo kwa muda mrefu amekua akisemekana kuwa amefulia na kuwa mlevi.
Kupitia ukurasa wake wa facebook, msanii huyo ameshare picha akiwa kwenye banda la kuku na kuandika;
“Sio mpaka niimbe tu ndio nipate hela. Hii pia ni moja ya kazi zinazonipa jeuri, sometime nakaa kimya kabisa ila sherehe zinaendelea na wengine wanahisi ninabiashara haramu. Napenda kuwashauri wasanii wenzangu mkishatoka kwenye majukwaa kile mnachokipata wekezeni kidogo ili msiwe watumwa na vipaji vyenu kwamba lazima uimbe ndio upate pesa”
Sisi wasanii wa Tanzania tunaweza kujimiliki lakini wengi wanapenda kumilikiwa ndo maana unakuta mtu kuanzia nyumba, gari hadi godoro analolalia kumbe sio lake. Nashukuru kwenye mkumbo huo sijawahi ingia na nadhani wapo wasanii wachache pia ambao hawajawahi ingia hasa hawa wa Hip Hop walio wengi nawafahamu itikadi zao kumilikiwa ni mwiko, ila wa bongofleva na bongomovie wengi wanapenda kitonga ndio maana hawafanikiwi. Kwa kasi ya JP Magufuli mnatakiwa mbadilike, kauli ya Hapa Kazi Tu itawanyoosha. Huu ni moja ya waraka wangu wa kishujaa na hauna chenga hata moja ni moja ya ujumbe wangu kwa mashabiki wangu.
Ambapo pia kwa muda mrefu kulikua na tetesi yakwamba Mr Nice amefulia, lakini kuonesha hajafulia hivi karibuni hitmaker huyo wa ‘Fagilia’ alionesha mjengo wake wake uliopo Chanika jijini Dar es salaam.
Tazama picha hapa chini zikimuonesha akihudumia kuku;
Leave your comment