EXCLUSIVE (TANZANIA) – Nisingekuwa hapa nilipo bila Lollipop – Mo Music

 

 

Msanii anayetamba na kibao cha ‘Basi Nenda’ Moshi Katema maarufu kama Mo Music, amesema kuwa bila ya kufanya kazi na mtayarishaji na mwandishi wa nyimbo Lollipop angeweza kuchukua muda mrefu sana kuwa na mafanikio aliyonayo kwa sasa.

Lollipop ndiye mwandishi wa ‘Basi Nenda’ pamoja na wimbo mpya alioutoa Mo Music hivi karibuni wa ‘Skendo’. Ambapo 'Basi Nenda' ndiyo iliyomfungulia milango kwenye fani ya Bongo Fleva.

“Lollipop anajua uwezo wangu wa uimbaji ukoje na ananisapoti sana, bila Lollipop nafikiri Mo Music angechelewa sana, kuanzia kwenye 'Basi Nenda' mpaka sasa hivi ushirikiano wake ni 90%”. Alisema Mo Music kupitia Planet Bongo ya East Afrika Radio.

Pia aliongeza kuwa wimbo wake mpya wa ‘Skendo’ anautabiria kufanya vizuri sana.

“Skendo naitabiria kuwa mega hit, nafikiri imevunja rekodi ya nyimbo zangu zote ndani ya masaa manne kwasababu mimi huwa natathmini nyimbo zangu ndani ya masaa manne tangu niiachie” alieleza Mo Music.

Leave your comment