TANZANIA: Bongo Flava Haitopotea Leo Wala Kesho - Lameck Ditto

Hitmaker wa Moyo Sukuma Damu, Lameck Ditto, amesema muziki wa Bongo Flava utaendelea kudunda kwa karne kibao. Anaamini kuwa Kiswahili ni lugha inaoufanya muziki huo kuwa special.

“Bongo Flava ni Kiswahili, moja ya vitu vinavyoweka ladha kwenye muziki wetu wa Bongo Flava ni Kiswahili na Kiswahili bado kipo na kinazidi kukua, kuenea na kusambaa kila kukicha maeneo mbalimbali Afrika Mashariki na duniani kote,” Ditto amekiambia kipindi cha VMix cha Channel 10.

“Hivyo sioni kama muziki wetu unapungua ladha kama Kiswahili kinazidi kukua na kutumika maeneo mbalimbali kwa maana hiyo Bongo Flava haiwezi kupotea leo wala kesho.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news