TANZANIA: Rama Dee aelezea uhusiano wa umri mkubwa wa msanii na kuchuja kimuziki

 

Muimbaji wa R&B nchini, Rama Dee, amesema haamini iwapo kuna uhusiano wa umri mkubwa wa msanii na kuchuja kimuziki. Amedai kuwa imani hiyo hujengwa kutengeneza uoga na hali ya kutojiamini kwa wasanii hao, kitu ambacho anakipinga.

Amemtolea mfano rapper Jay Z, ambaye December 4, 2016 ametimiza miaka 47, kuwa licha ya umri mkubwa bado ni wa moto.

Kupitia Insagram, Rama Dee ameandika:

Jay ni Mwana Muziki mwenye umri mkubwa kuliko wana Muziki wengi Wa Tanzania, why unafanya kazi ya muziki ikifika miaka 3 unaambiwa zamu yako imeisha. Huu ni uvuvu wa kuendeleza vipaji, wakati mwengine Mwanamuziki anahitaji msaada kwenye muziki…. kuwa mwanamuziki ni baraka za Mungu! Propaganda ya kusema mwanamuziki huyu wakati wake umeisha ni propaganda za uwoga na ni siasa za maji taka! Ambazo hazina umuhimu wowote zaidi ya Uvivu wa kufikiri!

Nakumbuka Bosi wa Clouds Fm Ruge Mutahaba aliwahi kusema uwezo wa @jidejaydee umeisha anatakiwa awapatie kijiti wasanii wengine, ila kiukweli mmeona uwezo wa Mwana Dada huyu mpaka kufikia leo.

Ushauri:

Nafikiri sisi wasanii tunatakiwa kwenda mbele tuangalie Target zetu!

Kila Mkoa wa Tanzania ungepata wasanii zaidi ya 50 ambao watakuwa kwenye mzunguko itasaidia kukuza Ajira na vipaji kwa ujumla!

Mtazamo:

Kwa mtazamo wangu naona biashara ya muziki imekuwa kubwa ila bidhaa yake Inauzwa kwenye mfuko wa Rambo! Dreams encompass your career, your business, your music and your family too! It’s important to stand by your own morals and beliefs. If you want your dreams to become reality you have to focus on not just now but also in the more distant future.

Katika hatua nyingine, Rama Dee amesema amefurahi kusikia kuwa Ruge Mutahaba hupenda kazi zake licha ya agizo la kampuni hiyo la kutocheza nyimbo zake.

Ameandika, “Katika vitu ambavyo nashukuru kwanza nashukuru kwa kila mwaka kuongeza shabiki wa muziki wangu akiwepo Mkurugenzi wa Clouds Fm Ruge Mutahaba. Kwa mimi ku-appreciate Kazi yangu ni bora zaidi ya kucheza Mara 100 kazi zangu kwenye Radio yako kwa sababu hazijawahi kuchezwa! Nakupa hongera kwa kuwa muwazi na mjasiri kwenye kutambua watu wenye Vipaji na uwezo mkubwa kwenye tasnia hii Kama Rama Dee! Ubarikiwe sana.”

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment

Other news