UCHAMBUZI wa STEVE IWATTA kuhusu ALIKIBA na DIAMOND.

-na steve iwatta.
KUNA vita ya maneno kati ya makundi
mawili ya mashabiki wa Muziki wa Bongo
Fleva, wanaowashabikia wasanii Alikiba na
Nasibu Abdul ‘Diamond’, kila upande ukidai
mtu wao ndiye anajua zaidi kuliko
mwingine.
Ni mjadala mpana katika mitandao ya
kijamii, mitaani na hata miongoni mwa
wasanii wenyewe ambao kwa kificho au
waziwazi, wamewahi kuzungumzia nani
mkali katika wawili hao.
"ALIKIBA"
Alikiba ama King Kiba, ndiye wa kwanza
kuingia na kupata jina katika Muziki wa
Bongo Fleva, katikati ya miaka ya 2000
akiwa na singo yake ya kwanza,
Cinderella ndiyo ilimfungulia milango, kwani
alichomoza hadi juu ambako alidumu kwa
muda mrefu.
Huenda Diamond amewahi kuimba kwa
kuiga baadhi ya nyimbo za Alikiba, kwa
sababu yeye alianza kupata jina mwaka
2009, mwaka ambao mwenzake tayari
alishakuwa na albamu mtaani.
Unapotaka kufanya ulinganisho wa wawili
hawa ni lazima uchague unataka
kuwalinganisha nini,
mfano; sauti ,mafanikio, uwezo binafsi, mashabiki na nk. Vinginevyo unaweza
kujikuta umewekeza katika chuki au
ushabiki, kitu ambacho hakitakiwi. Kwa
mfano, vigumu kupata idadi kamili ya
mashabiki wa wasanii hao, ingawa
mapokeo ya kazi zao yanaweza
kumuongoza mtu kuelewa.
Kitu kimoja cha msingi ambacho wengi
wanakubaliana ni kwamba Alikiba ana
uwezo mkubwa wa kuimba na mwenye
sauti nzuri kuliko Diamond.
Na
Diamond
anafanya biashara ya muziki, ndiyo maana
anaonekana kuwa juu ya Alikiba ambaye
anafanya muziki kwa mazoea.
Katika ubora wake, Alikiba aliwahi kukutana
na mkali wa R&B duniani, R Kelly, katika
projekti iliyoitwa One8, ambapo wakali
nane wa Afrika walifanya ngoma moja
iliyoitwa Hands Across Africa ambao
walikuwa ni yeye, Fally Ipupa, 2Face, Amani,
Movaizhaleine, 4X4, Navio na JK.
Licha ya Kiba kufika nyumbani kwa R Kelly,
studio kwake, alishindwa kutumia
ushawishi wa msanii huyo mkubwa ili
aweze kumsaidia kuingia katika soko la
Marekani. Mbaya zaidi, alishindwa pia
kujitangaza kimataifa kupitia Fally Ipupa na
2Face ambao ni maarufu kuliko yeye.
Ambwene Yessaya ‘AY’ alimkutanisha
Diamond na Davido wa Nigeria na akafanya
naye Ngoma ya Number One Remix. Hapa
kijana yule wa Tandale hakutaka kuishia
kwa msanii huyo pekee, akaingia nchini
humo na kufanya kazi na wasanii karibu
wote wakubwa, wakiwemo waliofanikiwa
zaidi, P Square.
Hiyo imempa Diamond kujulikana zaidi na
kumfanya kuwa mmoja wa wasanii
wakubwa Afrika, kiasi cha wengi kuhitaji
kolabo naye kutoka Afrika Kusini,
Zimbabwe, Ivory Coast na kwingineko
Afrika.
Alikiba haonekani kuwekeza akili yake yote
katika muziki anaoufanya. Ni kama mtu
ambaye anafanya muziki kwa kujifurahisha
na siyo kufikia malengo ambayo mashabiki
wake wangependa aende. Ana uwezo
mkubwa nyuma ya Mic, lakini ameshindwa
kuutumia ili kuliteka soko.
Kiba anaridhika.
Katika uhalisia ni makosa kumshindanisha
na Diamond kwa sababu haoneshi kama ni
mshindani wake. Alipokuwa katika ziara
yake Ulaya, akaitumia nafasi adimu
aliyoipata kukutana na marehemu Papa
Wemba na kufanya naye wimbo.
Baada ya kuliweza soko la Afrika, Diamond
anaonekana wazi kulitamani la Ulaya na
Marekani na hii ndiyo sababu ya yeye kuwa
msanii anayelipwa zaidi kuliko wote kwa
sasa hapa Bongo.
Kiba hatafuti kolabo na watu wa nje kwa
vile anadhani ataonekana anamuiga
mwenzake, wakati katika maisha, kuiga vitu
vizuri na vya maendeleo ni jambo la
kupongezwa.
Hata hivyo, Kiba anayo nafasi ya kubadilika
ili aweze kuwa mshindani wa kweli wa
Diamond, vinginevyo asahau.

Leave your comment