TANZANIA:Shadoo asaini lebo ya VOA ya Linex

 

 

Msanii Shadoo ambaye kwa sasa amesainiwa na Linex chini ya Lebel yake ya Voice Of Africa, ameelezea kile kilichomfanya apotee kwa muda kwenye game, licha ya juhudi alizokuwa nazo kabla hajatoka.

Akiongea kwenye Planet Bongo leo alipokuwa akitambulisha wimbo wake mpya, Shadoo amesema matatizo aliyoyapata bosi wake aliyekuwa anamsimamia kzi zake kabla ya kukutana na Linex, yalimfanya apitie kipindi kigumu sana, na kupelekea kujiingiza kwenye mambo yasiyofaa, ingawa hakufikia hatua ya kutumia madawa ya kulevya.

"Bosi wangu wa mwanzo alipata matatizo, alifiwa na mkewe, baba yake, na duka lake likafungwa, so baada ya hapo nikawa na hali mbaya sana kimaisha, hata nyumbani kula ilikuwa ya tabu, nilikuwa na stress nikapitia mambo mengi sana magumu, ila sikutumia unga, ndio nikakutana na bro akanichukua", alisema Shadoo.

Shadoo ambaye kwa sasa ana kazi mpya, amesainiwa na Linex kwenye lebo yake, na kufanya kuwa msanii wa pili wa lebo hiyo kwani kwa muda mrefu alikuwa peke yake.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment