TANZANIA: Audio zinaishi kuliko video - Billnas

 

 

 

Msanii Bill Nas ambaye kwa sasa anafanya poa na ngoma yake 'Chafu pozi' amefunguka na kusema kuwa yeye katika muziki anawekeza nguvu kubwa zaidi kwenye kutengeneza 'Audio' kuliko video kwani anadai 'Audio' zinaweza kuishi siku zote kuliko video.

Bill Nas alisema hayo jana kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kudai kuwa sababu kubwa ya nyimbo zake zote kuendelea kufanya vizuri na kukaa muda mrefu kwenye chati mbalimbali za vituo vya habari ni kutokana na jitihada zake na nguvu kubwa anayowekeza kwenye utengenezaji wa 'Audio' zake.

"Unajua siku zote muziki mzuri unaishi kuliko hata hizo video, maana unaweza kufanya video kali leo lakini baada ya miaka kadhaa ikawa imepitwa na wakati lakini ukifanya 'Audio' nzuri itaendelea siku zote ndiyo maana unaona leo hii kuna kazi nyingi za Albert Mangwea bado zinafanya vizuri. Hata mimi kazi zangu zinakaa muda mrefu kwenye chati mbalimbali sababu huwa naweka nguvu kubwa kutengeneza kazi nzuri ambazo zinapendwa na watu na hazichoshi kusikiliza" alisema Bill Nas.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment