TANZANIA: Ruby amzingua Motra the Future

 

 

 

 

Msanii wa bongo fleva Ruby ambaye siku za karibuni aliingia kwenye headline baada ya kutotokea kwenye video ya wimbo wa 'Yamoto Band' unaofahamika kama 'Suu' ambao alikuwa ameshirikishwa na kundi hilo na kuseme kwamba alikuwa busy. Video hiyo kutokana na kuwa na 'Stress' jambo ambalo yeye mwenyewe kupitia kipindi cha Planet bongo alikanusha na kusema kuwa alikuwa busy na mambo yake, hivyo Yamoto band hawakuona umuhimu wake ndiyo maana walishindwa kumsubiri.

Msanii huyo ameripotiwa tena kuchomoa kufanya video ya Rapper anayechipukia Motra the Future ambaye amemshirikisha katika wimbo wake 'One day' Motra The Future amedai kuwa alikuwa anategemea uwepo wa Rubby akiamini kuwa angekuwepo kwenye wimbo video hiyo ingeweza kumsaidia kufika mbali zaidi, lakini anadai toka awali Ruby alishamwambia kuwa anatakiwa kutafuta model.

 

 

"Dhumuni kubwa la mimi kung'ang'ania Ruby aendelee kubaki kwenye ile Chorus nilikuwa naamini kuwa wimbo huu ungenifikisha mbali sana kwa kuwa yeye tayari alikuwa amefika katika hatua ambayo wasanii wengi tulikuwa tunahitaji kufika, nilihisi Ruby kuwepo kwenye video ingenifikisha mbali zaidi kwa sababu Audio ilifika mbali nikajua tukifanya na video ingefika mbali zaidi"alisema Motra

Motra anasema yeye bado anamuheshimu Ruby kwani ni kama dada yake, ambaye wana heshimiana yeye anaamini kuwa labda kweli Ruby ametingwa na majukumu ya kila siku kiasi cha kukosa muda wa kwenda kufanya video ya wimbo huo.

"Yule ni kama dada yangu ambaye tunaheshimiana, naamini ni majukumu yamekuwa mengi zaidi kwani naamimi hata mimi labda itafika wakati nitakuwa msanii mkubwa na kuwa bussy na kazi, kiasi cha watu kuhitaji kufanya kazi na mimi wakati huo labda niko taiti na mambo mengine, inawezekana kweli yupo busy na mambo mengine lakini toka mwanzo alishaniambia kuwa nitafute model wa kuwepo kwenye video yangu na mimi nikaona haina noma kwa kuwa yeye ni mtu mzima, labda hakuona umuhimu wa mimi kuwepo pale." aliongeza Motra The Future

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment