Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: Hata kama wakikataa script hii ya ‘Chura’ tutawapelekea nyingine – Meneja wa Snura
17 July 2016

Meneja wa Snura, HK amedai kuwa hata kama serikali wakiikataa script ya video ya ‘Chura’ waliyoipeleka ikikataliwa bado wataendelea kupeleka nyingine.
Akiongea na Bongo5, HK amesema, “Hata wakiikataa hii script ya pili tutawapelekea script nyingine.”
“Tumeshapeleka script nyingine zaidi ya wiki tatu zilizopita na nimewapigia simu jana wameniambia bado hata kuipitia bado hawajaipitia. Tulikubaliana na serikali kuwa ni lazima video ya ‘Chura’ ifanyike,” alisema HK.
“Script tuliyowapelekea ni ya kawaida sana, kama wataikataa itabidi tuziweke zote mbili hadharani ili watu wachangie kwa kuwa hata ile ya kwanza haikuwa mbaya, walisema kuwa haina ujumbe kwahiyo kwenye script ya sasa hivi tumezingatia maamuzi yao waliyoyataka kwenye script hiyo,” ameongeza.
Hivi karibuni Snura ameachia wimbo wake mpya ‘Shindu’ ambao unazidi kufanya vizuri kwenye redio na mitaani pia.
Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz
Weekly Top 10 songs
Top stories
- Morning guys
16 August
- Kadric m Gangsta Bleed out Now
16 August
- Gan theking
16 August




Leave your comment