TANZANIA: Soggy Doggy ataja wasanii 3 wa RnB anaowakubali Tanzania

 

Msanii mkongwe wa muziki na mtangazaji, Soggy Doggy amefunguka kwa kudai kuwa wasanii wake bora wa muziki wa R&B ni Rama Dee, Nuruelly pamoja na Belle 9 na wengine walio baki wanaishi kwa promo tu na sio uwezo.

Akiongea katika kipindi cha Enewz kinachoruka katika runinga ya East Africa Television, Soggy Doggy amesema kukaa kwake kwa P Funky Majani kama producer msaidizi kumemfanya awatambue wasani ambao hawana vipaji.

“Mimi nashangaa watu wanajipa sana maflag, mwanamuziki mzuri wa R&B Tanzania nakutajia tatu bora yangu, namba moja ni Rama Dee, namba mbili ni Nuruhelly na namba tatu ni Belle 9,” alisema Belle. “Lakini kuna watu wengine wanapewa mipromo, mimi nimekaa studio nimekaa studio Bongo Record kama producer msaidizi wa P Funk, kwa hiyo mimi namjua mtu akiimba kwenye key au akitoka, najua sauti ya mtu,”

 

Nuruelly

 

Rama Dee

 

Belle 9

 

 

Aliongeza, “Jamani kuna watu wanaimba, ukimsikiliza Rama anaimba, ukimsikiliza Nuruelly bad news, lakini huwezi kumkuta mtu anampa attention kidogo, mtu anasubiri aimbe kama Wanigeria, so hii imesababisha watu wenye vipaji vyao kufanya mambo mengine,”

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment