TANZANIA: Simba kumshangilia Yanga? Thubutuuuuu" – Soggy Doggy

 

 

Msanii mkongwe katika wa muzuki wa bongo fleva, Soggy Doggy amefunguka na kusema kuwa mashabiki wa Simba kumshangilia Yanga hicho ni kitu kisichowezekana hata kidogo anasema kuwa yeye ni shabiki wa Simba damu

Msanii Soggy Doggy akiwa ametinga jezi ya TP Mazembe, yeye ni shabiki wa Simba kwa timu za nyumbani.

Hivyo leo atakwenda uwanja wa Taifa na kuishangilia timu ya TP Mazembe kutoka nchini Congo lakini si kuishangilia timu ya Yanga.

Soggy Doggy ameonyesha wazi kwa kununua jezi ya TP Mazembe na kuitinga huku akiandika maneno haya kwenye ukurasa wake wa Instgram na kusema kama watu wote wataishangilia Yanga nani ataishangilia timu hiyo ya TP Mazembe kutoka nchini DRC Congo.

"Wote tukiwa Yanga nani atawashabikia wageni? Kwa moyo mkunjufu kabisa nimejitolea kuwashangilia TP Mazembe. ...Simba kumshangilia Yanga? Thubutuuuuu" aliandika kwa msisitizo kabisa.

Na kwa upande wa Mwana FA anasema alikwenda uwanja wa ndege kuonana na Thomas Ulimwengu kwa kazi maalum moja tu kuhakikisha mjini hapa hakuna kelele baada ya mechi kati ya Yanga na TP Mazembe ambayo inachezwa leo. Na alikabidhiwa jezi ya TP Mazembe hivyo na yeye ni shabiki wa TP Mazembe leo.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment