TANZANIA: Ulaya itanipotezea soko la muziki - Linex

 

 

Msanii wa bongo fleva Linex Sunday Mjeda amefunguka ndani ya Enews kuhusiana na maneno yanayoendelea mitandaoni kuhusiana na kumwagana na aliyekuwa mpenzi wake ambaye pia alimshirikisha kwenye video ya wimbo wake wa 'Kwa Hela' kama video queen

Hata hivyo Linex anadaiwa kuwa na mahusiano na mwanamke wa kizungu na Enews ilitaka kujua kama bado anaendelea na mmarekani huyo na nini malengo yake kwa sasa, ambapo Linex alisema hajawahi kuachana na mpenzi wake huyo wa kizungu.

Linex pia amesema sababu za yeye kutoenda kuishi na mzungu wake Marekani ambapo amedai kwamba sababu kubwa ni kuhofia kupoteza soko lake la kimuziki hapa nchini huku akisisitiza kwamba alitumia nguvu nyingi sana kutangaza muziki wake hapa bongo, hivyo hataki kupoteza heshima yake ya muziki na kwamba mpezi wake huyo huja mara kwa mara nchini.

Baadhi ya watu wamekuwa wakimdisi sana Linex juu ya suti zake ambazo amekuwa akizivaa katika video zake na kusema kuwa suti hizo huwa zinamvaa na hapendezi.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment