TANZANIA: Ni kweli nilikuwa nikitumia madawa ya kulevya kwa zaidi ya mwaka sasa – Young Dee

 

Rapper kutoka bongoflevani Young Dee amerudi rasmi kwenye uongozi wake wa zamani wa MDB Record ambao uko chini ya Maximilian Rioba, miongoni mwa vitu alivyoviongea rapper huyo ni pamoja na kukiri kutumia dawa za kulevya kwa mwaka mmoja na miezi minne.

Mbele ya Waandishi wa habari, Young Dee amesema “Young Dee mnayemuona sasa hivi  sio yule wa zamani ambaye alikuwa akitrend kwenye mitandao ya kijamii kweli nilikuwa nikitumia madawa ya kulevya kwazaidi ya mwaka sasa, lakini ninachomshuuru mungu nikuwa siku fikia hali yampaka nipelekwe Rehab”.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment