TANZANIA: Bado nipo nipo – Dully Sykes

 

Baada ya kupost picha akiwa na Mwana FA baada ya kuoa na kuandika maneno yanayoashiria naye hivi karibuni atafuata nyayo za Mwana Fa, Dully Sykes ameruka viunzi na kusema hana mpango wa kuvuta jiko leo wala kesho.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dully amesema yeye kwake kuoa ni sawa na maji kufuata mkondo, kwana hata marehemu baba yake hakuwahi kuoa wakati wa uhai wake.

“Kila mtu ana mipango yake, maji hufuata mkondo, wewe nafikiri mzazi wako alioa, mi baba yangu hakuwahi kuoa”, alisikika Dully akielezea sababu ya yeye kutoamua kuoa mpaka leo.

Pamoja na hayo Dully amesema akiona kuna umuhimu na ikiwezekana ataoa, hivyo amewataka wadau wake wamuombee ili aweze kuwa na mawazo ya kuoa na kuwa na mke rasmi.

“Kama inawezekana naweza kuvuta jiko, na kama haitowezekana sitavuta jiko, kwa sababu sijafikiria bado, mniombee nipate mawazo ya kuchukua jiko, sio kwa vile FA amefanya basi ndo uone inawezekana, nina sababu zangu tu mwenyewe, nikikwambia ntakuvunja moyo kama umeoa wewe”, alisema Dully Sykes.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment